Saturday, 23 August 2025

CHAN 2024: Tanzania, Kenya zafungasha virago.


Timu za taifa za Kenya na Tanzania zimeaga mashindano ya CHAN baada ya kufungwa katika mechi za robo fainali. 

Katika mechi ya awali iliyochezwa katika uga wa Kasrani jijini Nairobi

Kenya ilitolewa na Madagascar kupitia mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.


Tanzania imepoteza mchezo ndani ya dakika 90 katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kufungwa goli moja bila majibu.

Sasa matumaini yote ya wenyeji yanaelekezwa Uganda ambao wanashuka dimbani kesho dhidi ya Senegal.

Kenya walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Alphonse Omoja dakika ya 38, kabla ya Razafimahatratra wa Madagascar kusawazisha dakika ya 60.

Baada ya kutoka ya sare ya 1-1 katika dakika 120, Madagascar walishinda 4-3 kwa mikwaju ya penalti, huku Toky Rakotondraibe akifunga mkwaju wa penalti baada ya Alphonce Omija kukosa.

Harambee Stars, ilikuwa ikiwania kutinga nusu fainali ya kwanza ya bara baada ya miaka 38.


No comments:

Post a Comment

Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...

Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker

Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini

Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini