Maelfu ya Wapalestina wamelazimika kuondoka Gaza City kufuatia mashambulizi ya Israel. Watu zaidi ya 16 wameuawa huku sehemu kubwa ya mji huo ikiachwa bila umeme baada ya Israel kushambulia miundombinu muhimu.
Mashambulizi makubwa katika jiji la Gaza yamepelekea maelfu ya watu kulazimika kuyahama makazi yao baada ya kuamriwa na jeshi la Israel. Msemaji wa Shirika la Kimataifa la kuwahudumia watoto UNICEF Tess Ingram ameiambia DW akiwa kusini mwa Gaza huko al Mawasi kuwa familia za Wapalestina zimeathiriwa na kuchoshwa na hatua hiyo ya kuhamishwa kila mara.
"Sheria ya kimataifa iko wazi. Watu lazima walindwe iwe wanaondoka au wameamua kubaki. Lakini kwa bahati mbaya, mara nyingi mno katika mzozo huu, tumeshuhudia sheria hizo za kimataifa zikipuuzwa, " aliongeza Tess Ingram.
Operesheni hiyo katika jiji la Gaza iliyoanza Jumanne na kuendelea Alhamisi, imeuchochea mzozo wa Mashariki ya Kati na kufifisha uwezekano wa kufikiwa mpango wa usitishaji mapigano. Jeshi la Israel ambalo limesema linalenga "kuharibu miundombinu ya kijeshi ya Hamas" halijaeleza shambulio hilo litadumu kwa muda gani lakini dalili zinaonyesha kuwa linaweza kuchukua miezi kadhaa.

No comments:
Post a Comment
Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...
Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker
Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini
Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini