Thursday, 18 September 2025

MERZ ATAKA WAJERUMANI WAJIANDAE KWA MABADILIKO.


Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amewataka raia wa Ujerumani wajiandae kwa mabadiliko makubwa katika miezi michache ijayo.
Merz ameyasema haya wakati serikali yake inapojiandaa kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto chungunzima zinazoikabili Ujerumani, ambayo ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa zaidi Ulaya.

Mojawapo ya changamoto kubwa zaidi kwa Merzna mawaziri wake zitakuwa kupata njia za kuirejesha Ujerumani katika ukuaji wa uchumi baada ya miaka miwili mfululizo ya mfumko wa bei.

Biashara zinazidi kupitia kipindi kigumu kutokana na bei ya juu ya nishati, kupungua kwa wateja na ushuru mpya wa Marekani, huku wengi wakiendelea kupunguza makadirio yao na nafasi za ajira ili kukabiliana na hali hiyo.

Merz aliyekuwa analihutubia bunge wakati wa wiki ya bajeti, amekiri kuhusiana na ugumu wa hali.

"Maamuzi yaliyo mbele yetu hayahusu mambo maalum, bali masuala muhimu," alisema Merz. "Si kuhusu kitu chengine chochote bali mustakabali wa nchi yetu - jinsi tunavyoishi, jinsi tunavyoishi pamoja, tunavyofanya kazi, tunavyofanya biashara na jinsi tutakavyoendeleza maadili yetu."

No comments:

Post a Comment

Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...

Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker

Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini

Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini