Kwa mara nyingine tena, mapingamizi yaliyowekwa na Lissu dhidi ya mwenendo wa mahakama kuhusu kesi yake ya uhaini, yamegonga mwamba baada ya Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Dar es Salaam kuyatupilia mbali na kuamuru kesi hiyo iende mbele katika hatua ya kusoma mashtaka.
Lissu aliweka mapingamizi matano akitaka kesi hiyo isiendelee kusikilizwa katika mahakama hiyo.
Hoja alizozitoa Lissu ni pamoja na mwenendo wa Mahakama ya Hakimu Mkaazi ya Kisutu kuahirisha kesi hiyo mara 13, kufichwa kwa mashahidi yeye kama mshitakiwa kutoruhusiwa kuwataja mashahidi wake, kutokupewa nyaraka za mwenendo wa kesi yake na nyaraka hizo kuchezewa.
Jaji atupilia mbali mapingamizi ya Lissu
Jaji Kiongozi kwenye kesi hiyo Dunstan Ndunguru lakini ameyatupilia mbali mapingamizi yote akisema hata kama ni kweli kuwa mashahidi wa Lissu hawakurekodiwa lakini hilo haliondoi mamlaka ya mahakama hiyo kuisikiliza kesi hiyo.
Na kuhusu hoja ya mkanganyiko wa tarehe za kesi kwenye nyaraka, Jaji Ndunguru amehitimisha kwa kusema ni makosa yaliyotokana na kalamu.
Lissu aliwasilisha mapingamizi hayo mahakamani Septemba 8, 2025 akihoji ikiwa Mahakama Kuu, Masijala Ndogo Dar es Salaam ina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhaini.
Jaji Ndunguru hatimaye aliahirisha kesi hiyo hadi saa 8:00 za mchana, ambapo itaendelea kwa upande wa mashtaka kumsomea hati ya mashtaka mshtakiwa.
Mapema, polisi waliwadhibiti vikali wafuasi wa CHADEMA na kuwajeruhi baadhi yao wakati wafuasi hao waliposhinikiza kuingia mahakamani. Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniphace Mwabukusi amelaani vikali vitendo hivyo vya jeshi la polisi na kusema watatoa tamko hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment
Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...
Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker
Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini
Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini