|
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi
huko Monduli, Arusha. Jeshi hilo litaadhimisha miaka 52 ya kuanzishwa
kwake Septemba Mosi kwa kufanya usafi katika mitaa mbalimbali ya nchi. |
Tarehe 1 Septemba wiki hii itakuwa siku ya aina yake nchini
kutokana na kubeba matukio makubwa manne moja likiwa la kimataifa
litakalofanya macho mengi duniani kuelekezwa Tanzania. Matukio
hayo ni kupatwa kwa jua kitendo kitakachotokea kwenye usawa wa anga ya
Tanzania katika eneo la Rujewa mkoani Mbeya na lile la Waziri Mkuu
kuhamia rasmi Dodoma ikiwa ni kutekeleza ahadi yake aliyoitoa mara baada
ya Rais John Magufuli kutangaza azma ya Serikali yake kuhamia huko
katika kipindi cha miaka minne na ushee ya utawala wake kilichobaki.