Thursday 3 November 2016

UEFA: MADRID YABANWA UGENINI.

Wachezaji wa Madrid wakishangilia goli la Bale

Klabu bingwa barani Ulaya imeendelea usiku wa kuamkia leo ikiwa bado katika hatua za makundi.
Mchezo wa kusisimua zaidi ukiwa kati ya Legia Warsaw dhidi ya Real Madrid ambao ulikuwa wa piga nikupige.
Huku ikishuhudiwa Gareth Bale akifunga goli la kusisimua zaidi. Matokeo ya mwisho Legia Warsaw 3-3 Real Madrid.
Mchezo huo ulikuwa bila ya mashabiki wa Legia baada ya kufungiwa na Uefa.
Monaco ikiwa nyumbani imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya CSKA ya Moscow.
Tottenham Hotspur pia ikiwa nyumbani katika dimba la Wembley ilikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Tottenham walitumia uwanja wa Wembley badala ya White Hart Lane
Leicester City ikiwa ugenini ililazimishwa sare tasa dhidi ya FC Copenhagen.

Matokeo ya michezo mingine

Borussia Dortmund 1-0 Sporting
FC Copenhagen 0-0 Leicester city
FC Porto 1-0 Club Brugge
Juventus 1-1 Lyon1
Sevilla 4-0 Dinamo Zagreb

No comments:

Post a Comment

Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...

Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker

Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini

Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini