LIGI Kuu Bara inaendelea tena leo kwa mechi moja kupigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga kuanzia saa 1:00 usiku na wenyeji Coastal Union iliyoanza na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons, itakuwa na vita kali na maafande wengine wa JKT Tanzania walioanza kwa sare ya 1-1.
Coastal ilianza Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons Septemba 17, 2025, huku kwa upande wa JKT Tanzania ikilazimishwa sare ya 1-1 na Mashujaa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, Septemba 18, 2025.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa Coastal Union, Ali Mohammed Ameir alisema licha ya kuanza vyema mechi ya kwanza dhidi ya Prisons, ila bado hakuridhishwa na eneo la ushambuliaji, kutokana na nafasi nyingi za kufunga zilizotengenezwa.
“Ligi ni ngumu kwa sababu kila mpinzani tunayekutana naye amejipanga pia, tumeanza vizuri na tunahitaji kuendelea hivyo, tupo nyumbani na tunapaswa kutumia hiyo faida kwa sababu tutakapoanza kutoka ugenini haitokuwa rahisi,” alisema Ameir.
Kwa upande wa Kocha wa JKT Tanzania, Ahmad Ally alisema siyo rahisi kucheza mechi mbili mfululizo ugenini, kutokana na ushindani uliopo, ingawa jambo analofurahia ni kuona wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wako fiti licha ya uchomvu tu.
Mechi hii ya leo ni ya kisasi kwa JKT ambayo mara ya mwisho ilipokutana na Coastal ilichapwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Februari 7, 2025, licha ya raundi ya kwanza timu hiyo kushinda 2-1, Septemba 25, 2024.
Katika mechi mbili za msimu uliopita za Ligi Kuu Bara ambazo timu hizo zimekutana, yameshuhudiwa mabao sita yakifungwa, jambo linaloonyesha zina safu kali ya ushambuliaji, ingawa kwenye eneo la kujilinda pande zote mbili bado ni changamoto.
Timu zote zinakutana zikiwa na mastaa wapya, lakini wenyeji wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuanza msimu na ushindi nyumbani, ingawa JKT iliyomaliza ya sita msimu uliopita haitabiriki chini ya kocha Ahmad Ally.

No comments:
Post a Comment
Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...
Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker
Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini
Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini