Monday, 22 September 2025

RAIS WA ZAMANI MUTHARIKA AONGOZA, MATOKEO MALAWI.


Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika anaongoza katika matokeo ya uchaguzi uliofanyika wiki hii dhidi ya mpinzani wake wa karibu rais wa sasa Lazarus Chakwera.
Matokeo ya awali ya robo moja ya kura zilizohesababiwa yanampa Mutharika asilimia 51 ya kura ya mabaraza tisa kati ya 36 ya nchi nzima huku Chakwera akishikilia asilimia 39 kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters ambalo limefanya mahesababu kwa kuzingatia matokeo yaliyochapishwa na tume ya uchaguzi.


Mgombea atakayeshinda moja kwa moja uchaguzi nchini humo anahitaji kuchaguliwa na zaidi ya asilimia 51 ya kura halali vinginevyo kutaitishwa duru ya pili ya uchaguzi.

Wachambuzi wa kisiasa walishatabiri kwamba uchaguzi huo uliofanyika Septemba 16 utakuwa ni mpambano kati ya vigogo hao wawili wa vyama vikubwa vya kisiasa katika bunge la Malawi, Mutharika na Chakwera.
Hali ngumu ya kiuchumi itamponza Chakwera?

Nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika inakabiliwa kwa sasa na hali ya mkwamo wa kiuchumi tangu mchungaji Chakwera mwenye umri wa miaka 70 alipochaguliwa kuwa rais miaka 5 iliyopita.

Hali ngumu ya maisha imezidishwa na majanga yanayohusishwa na mabadiliko ya tabia nchi yaliyowahi kupiga malawi ya kimbunga na ukame. Kiwango cha mfumko wa bei unaoshuhudiwa Malawi ni zaidi ya asilimia 20 kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu.

Rais wa zamani Peter Mutharika mwenye umri wa miaka 85 aliyewahi kuwa profesa wa sheria alisifiwa kwa kuimarisha miundo mbinu na kupunguza mfumko wa bei wakati alipokuwa madarakani mwaka kuanzia 2014 hadi 2020, lakini wanaomkosoa wanasema ni mtu mwenye upendeleo kwa jamaa zake hata kwa wasiokuwa na uwezo.

Hata hivyo Chakwera alipoingia madarakani baada ya Mutharika mnamo mwaka 2020 aliahidi kupambana na kuimaliza rushwa amekuwa akikosolewa kwa namna anavyoshughulikia kesi za rushwa akishutumiwa kuchagua yule wa kumuandama lakini pia kwa kufuatia rushwa kwa mwendo wa kinyonga.


Tume ya uchaguzi ina muda wa hadi Septemba 24 kutangaza matokeo kamili ya awali ya uchaguzi huo wa rais na imetowa onyo dhidi ya wagombea kujitangazia ushindi kabla ya tume. Imesema inahakiki na kukusanya matokeo yote yaliyokwisha hesababiwa ili kuhakikisha hakuna dosari.

Itakumbukwa kwamba mahakama ya katiba katika uchaguzi wa mwaka 2019 uliyafuta matokeo yaliyompa ushindi Peter Mutharika kutokana na dosari zilizotokea ikiwemo kuthibitishwa kwamba ulitumika wino wa kufanya marekebisho kwenye karatasi za matokeo.

Kutokana na uamuzi huo wa mahakama ya katiba, baadae Chakwera alishinda uchaguzi uliorudiwa mnamo mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment

Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...

Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker

Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini

Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini