Monday, 22 September 2025

CHAMA TAWALA MALAWI CHALALAMIKIA WIZI WA KURA.



Chama tawala Malawi cha Rais Lazarus Chakwera cha Malawi Congress, MCP, kimedai kina ushahidi wa wizi wa kura, wakati ambapo matokeo ya awali yanaashiria kuwa kinashindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi habari, Vitumbiko Mumba, mgombea mwenza wa Rais Chakwera, amesema wana ushahidi kuwa baadhi ya watu walikuwa wanajaza karatasi bandia za kupigia kura kwenye masanduku ya kura.

Kwa mujibu wa Mumba, mwanasiasa wa chama cha MCP matokeo ya awali hayalingani na takwimu zilizotangazwa katika kituo cha kuhesabia na kujumlisha kura.

Hata hivyo, chama hicho hakijaonyesha ushahidi wowote ule wa tuhuma hizo.

Mumba amesema chama cha MCP, kimewasilisha malalamiko yake katika Tume ya Uchaguzi ya Malawi, MEC.

Tume hiyo ina muda wa hadi Septemba 24, kutangaza matokeo rasmi ya urais.

No comments:

Post a Comment

Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...

Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker

Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini

Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini