Monday, 21 November 2016

SALAMU KWA LOWASSA ZAITA POLISI KIKAONI.


Polisi jana walihoji uhalali wa mkutano wa ndani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya kundi kubwa la watu kuzingira ofisi za Chadema kwa lengo la kumsalimia aliyekuwa mgombea wake urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Edward Lowassa.




Wananchi walitaka kumsalimia Lowassa baada ya kugundua ni mmoja wa viongozi wa chama hicho walio kikaoni, katika mji mdogo wa Kibaigwa, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
Akizungumza na Nipashe jana, Mwalimu alisema wakiwa wanaendelea na kikao cha ndani katika ofisi za chama hicho Kibaigwa, wananchi wengi walijitokeza baada ya kugundua Lowassa ni mmoja wa washiriki wa kikao hicho.

Lowassa ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, alikuwa na Makamu Mwenyekiti (Bara), Profesa Abdallah Safari, Naibu Katibu (Zanzibar), Salum Mwalimu na mbunge wa Rombo, Joseph Selasini.

Wengine walikuwepo katika mkugtano huo ni mbunge wa jimbo la Tunduma, Frank Mwanjala, Grace Kiwelu (mbunge wa viti maalum- Kilimanjaro), Konte Majala na Swale Semesi ambao wote wawili ni wabunge wa viti maalum mkoa wa Dodoma.

Mwalimu alisema hali hiyo ya mkusanyiko wa wananchi wengi katika ofisi hizo, iliwafanya polisi wa kituo cha Kibaigwa kufika na kuwahoji iwapo wana kibali cha kufanya mkutano.
“Nasi tuliwauliza polisi tangu lini kikao cha ndani kukawapo na kibali … kwa kutumia busara polisi hao waliondoka nasi tukiwa tunaendelea na kikao chetu,” alisema Mwalimu.

Alisema kikao hicho kilikuwa ni mikakati ya chama kuweza kujijenga kwa viongozi wao wa ngazi za wilaya na wale wa majimbo.
Alisema waliokusanyika maeneo hayo walikuwa na lengo la kuwasalimia.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ernest Kimola, alisema kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, hivyo waliingilia kikao cha viongozi hao ili kuhakikisha usalama wao kutokana na watu kukusanyika.

“Hiyo ni moja ya kazi yetu, tuliingilia kati baada ya kuona watu wamekusanyika walipo viongozi hao, lakini lengo letu lilikuwa ni kuhakikisha usalama wao kwanza,” alisema Kimola.

No comments:

Post a Comment

Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...

Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker

Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini

Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini