Thursday 28 February 2019

TAMISEMI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI 2019.

Ofisi ya Rais - TAMISEMI inapenda kuutangazia Umma kuwa Serikali imetoa kibali cha nafasi za ajira ya walimu ili kujaza nafasi wazi zilizopatikana kutokana na walimu waliofariki, walioacha kazi, waliofukuzwa utumishi na wastaafu kuanzia kipindi cha Julai, 2018 hadi Juni, 2019. Kwa sababu hiyo, OR-TAMISEMI imeandaa mfumo wa Online Teacher Employment Application System – OTEAS ambapo walimu wenye sifa watatuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha OTEAS

Walimu wanaotakiwa kutuma maombi ni wenye sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:


A. WALIMU WATAKAOAJIRIWA SHULE ZA MSINGI

  • Mwalimu Daraja la IIIA – mwenye Astashahada (Cheti) ya Ualimu;
  • Mwalimu Daraja la IIIB - mwenye Stashahada (Diploma ya Ualimu katika masomo ya English, Civics, Historia, Jiografia na Kiswahili;
  • Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu kwa masomo ya English, Civics, General Studies, History, Geography & Kiswahili.
  • Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Mahitaji Maalum aliyehitimu Shahada ya Ualimu kwa masomo ya English, Civics, General Studies, History, Geography & Kiswahili.
B. WALIMU WATAKAOAJIRIWA SHULE ZA SEKONDARI
  • Mwalimu Daraja la IIIC – mwenye Shahada ya Ualimu waliosomea Elimu Maalum;
  • Mwalimu Daraja la IIIB – mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu waliosomea Elimu Maalum;
  • Mwalimu Daraja la IIIB – mwenye Stashahada ya Ualimu somo la Physics, Mathematics , Biology & Chemistry;
  • Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Agriculture Science;
  • Mwalimu Daraja la IIIC – mwenye Shahada ya Ualimu somo la Home Economics;
  • Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Physics, Mathematics, Chemistry & Biology;
  • Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Book Keeping, Commerce, Accounts & Economics; na
  • Mwalimu Daraja la IIIC – mwenye Shahada ya Ualimu somo la English, Civics & General Studies.
C. SIFA ZA JUMLA
Waombaji wa nafasi tajwa hapo juu wawe na sifa za jumla zifuatazo:-
  • Awe ni Mtanzania;
  • Awe amehitimu chuo kinachotambulika na Serikali kati ya mwaka 2014 hadi 2017; isipokuwa kwa wahitimu wa Elimu ya Ualimu wa masomo ya Fizikia na Hisabati;
  • Asiwe na umri wa zaidi ya miaka arobaini na tano (45) wakati wa kutuma maombi haya;
  • Walimu waliowahi kutuma maombi na hawajaajiriwa wanapaswa kutuma maombi upya.

D. MWISHO

Maombi yote yawasilishwe kwa mtandao na yawe na nakala za vyeti vya taaluma, utaalamu na kuzaliwa. Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kuanzia tarehe 27/02/2019 hadi 15/03/2019.

Imetolewa na
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais - TAMISEMI

No comments:

Post a Comment

Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...

Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker

Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini

Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini