Monday, 22 September 2025

TRUMP ANAMSIFU CHARLIE KIRK KAMA 'SHUJAA WA MAREKANI' HUKU MAELFU WAKIFURIKA IBADA YA KUMBUKUMBU YAKE.


Rais wa Marekani Donald Trump alimsifu mwanaharakati wa kihafidhina na mshirika wake Charlie Kirk kama "shujaa mkuu wa Marekani" na "shahidi aliyefia dini" wakati wa hotuba kwa makumi ya maelfu ya waombolezaji katika ibada ya kumbukumbu huko Arizona kufuatia kuuawa kwake.

Trump alikuwa mzungumzaji mkuu katika hafla hiyo iliyojaa watu Jumapili, ambapo maafisa wakuu kutoka kwa utawala wake, akiwemo Makamu wa Rais JD Vance, walisifu urithi wa kisiasa wa Kirk baada ya kupigwa risasi tarehe 10 Septemba.

"Aliuawa kwa sababu aliishi kwa ujasiri, na alibishana kwa ustadi," Trump aliuambia umati katika uwanja wa State Farm karibu na Phoenix.

Mke wa Kirk, Erika, pia alitoa hotuba ya maombolezo iliyojawa simanzi alisema alimsamehe anayedaiwa kuwa muuaji wa mumewe.

"Mume wangu, Charlie, alitaka kuwaokoa vijana, sawa na yule aliyemuua," alisema, na kuongeza: "Ninamsamehe kwa sababu ndivyo Kristo alivyofanya. Jibu la chuki si chuki."

Makumi ya maelfu ya watu walipanga foleni kwa saa nyingi nje ya uwanja kabla ya tukio hilo, huku wengine wakipiga kambi usiku wa kuamkia jana ili kupata nafasi ya kumuomboleza. Wengi walivalia kofia za Make America Great Again (MAGA), na vitu vingine vyenye chapa ya Trump na mavazi nyekundu, nyeupe na bluu.

No comments:

Post a Comment

Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...

Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker

Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini

Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini