Hali ya kibinadamu katika mji wa El-Fasher nchini Sudan inazidi kuzorota baada ya mashambulizi mapya ya vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) yaliyosababisha vifo, utekaji na uharibifu mkubwa. Madaktari wamesema watu wasiopungua 13, wengi wao wanawake na watoto, waliuawa waliposhambuliwa wakiwa barabarani karibu na mji wa huo mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.Mtandao wa Madaktari wa Sudan (SDN) umesema mauaji hayo ni sehemu ya kampeni ya mauaji ya kikabila na mauaji ya halaiki yanayolenga raia wasio na silaha katika eneo la Darfur. Kundi hilo limeeleza kuwa miongoni mwa waliouawa walikuwemo watoto watano na wanawake wanne.
Shambulizi hilo lilitokea siku moja baada ya RSF kushambulia hospitali mjini El-Fasher ambako wafanyakazi wa afya na wagonjwa saba walijeruhiwa, akiwemo mtoto na mwanamke mjamzito.
Hospitali hiyo, moja ya tatu pekee zinazofanya kazi mjini humo, sasa imelazimika kusitisha huduma za dharura kutokana na uharibifu mkubwa.
RSF yauzingira mji wa El-Fasher kwa zaidi ya mwaka mmoja
Katika tukio jingine, wanamgambo wa RSF walivamia kambi ya wakimbizi ya Abu Shouk iliyo karibu na el-Fasher na kuwateka nyara raia wanane – wanawake sita, mtoto mchanga wa siku 40 na mtoto wa miaka mitatu. Vyanzo vya uokoaji vinasema zaidi ya watu 20 hawajulikani walipo, na idadi kamili ya waliotekwa huenda ikawa kubwa zaidi.
Mji wa el-Fasher, uliokuwa ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan magharibi mwa Darfur, umekuwa chini ya mzingiro wa RSF kwa zaidi ya mwaka mmoja. Wakati huo huo, kambi za wakimbizi ikiwemo Abu Shouk zimekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara, na wiki iliyopita familia moja ya watu watano waliuawa kwa shambulio la moja kwa moja kwenye makazi yao.
Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa mashambulizi ya kikatili ya RSF dhidi ya mji wa El Fasher na kambi ya Abu Souk, yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 89 katika kipindi cha siku 10 kufikia Agosti 20. Msemaji wa ofisi hiyo Jeremy Laurence, anasema huenda idadi halisi ya vifo vya raia ikawa kubwa zaidi.

No comments:
Post a Comment
Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...
Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker
Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini
Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini