
BAADA ya Denis Kitambi kutangazwa kukiongoza kikosi cha Fountain Gate, kocha huyo amesema kuanza vibaya msimu mpya wa 2025-2026, hakujawatoa katika malengo, licha ya kukiri pia ana kazi kubwa hususan ya kutengeneza muunganiko wa kikosi.
Kocha huyo aliyezifundisha timu kadha ikiwamo Simba, Namungo, Geita Gold na Singida Black Stars, amezungumza hayo baada ya kuanza Ligi Kuu Bara kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City mechi iliyopigwa Tanzanite Kwaraa, mkoani Manyara, Septemba 18, 2025.
“Tumeanza kwa changamoto ya kutokuwa na wachezaji wetu kamili kwa sababu ya tatizo la kimfumo, msimu huu tuna kikosi bora cha ushindani kinachohitaji muda wa kutengeneza balansi na muunganiko wa kiuchezaji,” alisema Kitambi.
Kocha huyo alisema kutokamilika kwa nyota wote na kushuhudia kikosi hicho kikiwa na wachezaji 14 katika mechi iliyopita na Mbeya City kwa kiasi kikubwa ilishusha morali ya timu, ingawa bado wana uwezo na nafasi ya kuendelea kupambana zaidi.
Baada ya kucheza na Mbeya City, uongozi wa Fountain Gate uliiandikia barua Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), kuiomba mechi zijazo zisogezwe mbele, ili wapate nafasi ya kushughulikia changamoto iliyojitokeza katika mfumo wa usajili wa kimataifa (TMS).
Kitambi amejiunga na timu hiyo akichukua nafasi ya Mnigeria Ortega Deniran, aliyeondoka mapema tu kabla ya msimu kuanza, akisaidiana na Mohamed Ismail ‘Laizer’ aliyekibakisha kikosi hicho Ligi Kuu Bara kwa mechi za ‘play-off’ dhidi ya Stand United.
Laizer aliiepusha timu hiyo na janga la kushuka daraja baada ya msimu wa 2024-2025, kumaliza Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya 14 na pointi 29, ikianza ‘Play-off’ ya kwanza kwa kutolewa na maafande wa Tanzania Prisons kwa jumla ya mabao 4-2.
Baada ya hapo, Fountain ikacheza tena ‘play-off’ nyingine na Stand United inayoshiriki Ligi ya Championship iliyomaliza nafasi ya tatu iliyoitoa Geita Gold ilijihakikishia kubakia Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla wa 5-1.
No comments:
Post a Comment
Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...
Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker
Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini
Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini