Wicknell Chivayo, si jina geni barani Afrika, amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina ya maisha ya kifahari anayoishi, pamoja na picha zake na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika.
Hivi karibuni, taarifa iliyodaiwa kutoka bodi ya kupambana na rushwa kutoka Zimbabwe ilisaambaa kupitia ukurasa wa X, ikisema kuwa uchunguzi dhidi yake umefunguliwa juu ya madai ya Rushwa.
Hata hivyo taarifa hiyo ilifutwa muda mfupi baadae kutoka katika ukurasa huo, lakini picha na nakala za tangazo hilo bado zinaendelea kusambaa mitandaoni. Mwezi juni mwaka huu bodi hiyo ya kupambana na rushwa ilitoa taarifa kuwa ukurasa wake wa X ulidukuliwa.
Lakini bwana Wicknell Chivayo kutoka Zimbabwe ni nani hasa?
Ana umri wa miaka 44, Ni Tajiri mwenye utata, mara nyingi anapenda kujiita ''Sir Wicknell"
Baadhi ya watu wanavutiwa naye, huku wengine wakihofia – kwa tabia yake ya kugawa magari na hela nyingi kwa wale anaowaona kama wazalendo, hata kwa watu ambao hajawahi kuonana nao.
Magari anayopendelea kugawa ni kama Mercedes-Benz, Toyota SUV na Range Rover. Wanaonufaika ni mastaa wa muziki, waimbaji wa injili wasio na uwezo, wachezaji wa mpira, viongozi wa makanisa na hata wale wanaoonesha uaminifu kwa chama tawala cha Zanu-PF.
Yeye mwenyewe hupenda kuendesha Rolls-Royce nyeupe na ana msururu wa magari ya kifahari yaliyowekwa majina yake. Baadhi ya magari hayo naye ameanza kuyatoa anaponunua modeli mpya.
![]() |
"Sir Wicknell", ambaye alianza 'mkata tiketi' wa mabasi, amekuwa mtu mashuhuri kiasi kwamba picha zake zimekuwa zinapamba magari ama usafiri wa umma |
Kwa miaka mingi "Sir Wicknell" – kama anavyojiita – amekuwa akipenda kujionesha utajiri wake kupitia Instagram, jambo ambalo magazeti ya udaku hufuatilia sana. Lakini pamoja na kuonyesha wazi jinsi anavyotumia pesa zake, hajawahi kueleza kwa uwazi anazipataje, jambo linalozua maswali mengi, nchini kwakwe na hata nchi nyingine za jirani.
Katika mwaka mmoja uliopita, mitandao yake ya kijamii pia imejaa sana posti za misaada na zawadi anazotoa.
Katika mwaka mmoja uliopita, mitandao yake ya kijamii pia imejaa sana posti za misaada na zawadi anazotoa.
Mara nyingi posti hizo zinafanana: picha ya gari jipya linalong'aa limepambwa na maputo – wakati mwingine hata likiwa na utepe mkubwa juu ya boneti – ikifuatwa na ujumbe wa kumpongeza mtu fulani na maelezo ya wapi aende kuchukua gari hilo, mara nyingi kutoka kwenye maduka ya magari ya kifahari anayoshirikiana nayo jijini Harare.
Amekua pia akionesha mapumziko yake ya likizo Dubai, New York, Paris, London na safari za kibiashara Johannesburg, Shanghai na New Delhi – na mwanzoni mwa mwaka aliweka posti kuhusu ndege yake mpya ya binafsi.
Anapenda pia kuonyesha jinsi alivyo karibu na watu wenye ushawishi wa kisiasa na madaraka – akiposti picha akiwa na wanasiasa, kuanzia Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, mrithi wake Emmerson Mnangagwa, hadi viongozi wengine wa Afrika hasa hivi karibuni kama Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na William Ruto wa Kenya.
![]() |
CHANZO CHA PICHA,WICKNELL CHIVAYO/INSTAGRAM Maelezo ya picha,Wicknell Chivayo akiwa na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera katika msururu wa mikutano yake na viongozi wa Afrika |
Katika kitabu cha kumbukumbu Cry Havoc cha mwaka 2011, kilichoandikwa na marehemu Simon Mann – askari wa zamani wa jeshi la Uingereza na mpangaji wa mapinduzi aliyewahi kufungwa Zimbabwe katika Gereza Kuu la Chikurubi – alieleza kwamba mfungwa mwenzake, Wicknell, ambaye alikuwa "amesoma vizuri", alimwonya asithubutu kukosoa chama cha Zanu-PF.
Urafiki wao uliendelea na mwaka 2013 Wicknell aliposti picha yao wakitabasamu pamoja – mwaka huo ulionekana kama mabadiliko makubwa kwake.
Ni mwaka huo ambapo, pamoja na kuingia Instagram, kampuni yake Intratrek Zimbabwe kwa kushirikiana na kampuni ya Kichina walishinda tenda ya kujenga mradi wa nishati ya jua wenye thamani ya $172.8 milioni.
Lakini mradi huo baadaye uligubikwa na madai ya ulaghai – rekodi za mahakama zikaonyesha Intratrek walilipwa fedha za kuanzia ili kuanza kazi ya mradi wa 100MW Gwanda, lakini wakashindwa kutekeleza ipasavyo kwa kampuni ya umeme ya serikali (ZPC).
Yeye kwa upande wake aliishtaki ZPC kwa kuvunja mkataba. Alishinda kesi hiyo na baadaye akasafishwa kwenye mashtaka ya jinai.
![]() |
CHANZO CHA PICHA,AFP/GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Akiwa gerezani kwa ulaghai, Wicknell Chivayo alianzisha urafiki na muingereza aliyetuhumiwa kwa njama ya mapinduzi Simon Mann, na kumpa ushauri. |
Sir Wicknell mara chache huongea na vyombo vya habari, anasema hapendi waandishi wa habari na alikataa mahojiano. Lakini mwaka jana, kwenye kipindi cha redio cha asubuhi, aliulizwa moja kwa moja chanzo cha pesa zake.
Kwa sauti ya aibu, alisema biashara zake kuu ni tenda za serikali alizoshinda kwa kushirikiana na wabia wa kigeni katika miradi ya nishati mbadala, uhandisi, ujenzi na miradi ya umeme. Aliongeza pia kuwa ana biashara Kenya, Afrika Kusini na Tanzania.
Mwishoni mwa mwaka jana, kampuni yake IMC Communications ilipewa leseni ya kuwa mshirika wa huduma ya intaneti ya setilaiti ya Starlink inayomilikiwa na Elon Musk.
Katika Instagram, mara nyingi hujiona kama mtu mwenye "mguso wa dhahabu" – akijiita hustler anayefanya kazi kwa bidii. Anasema pia amefanikiwa kama "milionea aliyepambana mwenyewe" kutokana na maisha yake ya utotoni katika mji wa Chitungwiza, ambako familia yake ilihangaika baada ya baba yake kufariki yeye akiwa na miaka 10 tu.
Mara kwa mara huchapisha picha za kumbukumbu akiwa kijana mdogo alipokuwa akifanya kazi ya kulipa mishahara katika kampuni ya mabasi kupitia rafiki wa familia. "Nakumbuka nilikuwa kijana pekee wa umri wangu niliyekuwa na simu ya mkononi Chitungwiza," amewahi kusema kuhusu bidii yake.
![]() |
CHANZO CHA PICHA,NURPHOTO/GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Wicknell Chivayo ni muumini wa kanisa la kitume, ambalo waumini wake hukusanyika nje na kuabudu wakiwa wamevalia mavazi meupe |
Mwanzoni mwa mwaka kulikua na gumzo kuhusu nyaraka zilizovuja zikihusishwa na mkataba wa $500 milioni wa kusambaza vifaa vya matibabu ya saratani kwa serikali ya Zimbabwe, ukimtaja Wicknell kama mkurugenzi wa kampuni husika.
Hasira kubwa ni kwamba, kama kweli upo, haukupitia mchakato wa zabuni ya umma. Serikali na Chivayo wamekanusha, wakisema huo "mkataba" ni waraka wa kugushi ambao haujasainiwa.
"Kwa makundi yote ya upinzani kushirikiana na kupiga kelele kuhusu waraka feki usiosainiwa ni aibu kubwa na ishara ya kukosa maana kisiasa," alisema Chivayo.
Baba wa watoto wawili huyu, ambaye hivi karibuni alifunga ndoa ya kifahari iliyohudhuriwa na zaidi ya wageni 15,000, mara nyingi amesema hana nia ya kuwa mwanasiasa.
Kwake yeye ni pesa tu – na anasema amedhamiria kuwashinda "wanaomchukia."
Lakini ukaribu wake na watawala na wanasiasa, ambao ndio umemfanya awe tajiri, unamaanisha atabaki kuwa na utata daima.
No comments:
Post a Comment
Subscribe My YouTube Channel Here:
https://www.youtube.com/channel/UCRdp...
Like My Facebook page:
https://www.facebook.com/lyizzmaker
Follow Me On Twitter:
https://www.twitter.com/habariyamjini
Follow Me on Instagram:
https://www.instagram.com/habariyamjini