Mgombea urais kupitia Chama cha NCCR-Magezi, Haji Khamis ameahidi kusimamia maadili ya uongozi na kuwawajibisha viongozi watakaobainika kutumia ofisi za umma kwa manufaa binafsi, endapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao.
Wicknell Chivayo, si jina geni barani Afrika, amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina ya maisha ya kifahari anayoishi, pamoja na picha zake na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika.
Mahakama Kuu nchini Tanzania imetupilia mbali mapingamizi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kuhusu makosa aliyoyabaini katika hati ya mashitaka na hitilafu katika viambatanisho vya hati ya mashitaka.
Nianze kwa kukumbusha kilichotokea nchini Kenya katika uchaguzi wa 2022. Miongoni mwa wagombea wa kiti cha urais, kulikuwa na mtu akiitwa George Wajackoyah, ambaye ni wakili na profesa wa sheria, chini ya chama cha Roots.
Chama tawala Malawi cha Rais Lazarus Chakwera cha Malawi Congress, MCP, kimedai kina ushahidi wa wizi wa kura, wakati ambapo matokeo ya awali yanaashiria kuwa kinashindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita.
Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika anaongoza katika matokeo ya uchaguzi uliofanyika wiki hii dhidi ya mpinzani wake wa karibu rais wa sasa Lazarus Chakwera.
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema)Tundu Lissu, itaendelea leo katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Kwa zaidi ya robo karne, jina la Maalim Seif Sharif Hamad lilihusiana moja kwa moja na siasa za upinzani Zanzibar. Kwa wafuasi wake, alikuwa alama ya matumaini; kwa wapinzani wake, alikuwa mpinzani sugu, asiyechoka, ambaye mara zote aliamini kuna nafasi ya mabadiliko.
Mvutano waibuka kwenye Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Dar es Salaam baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kugoma kuendelea na shauri la uhaini akishinikiza wafuasi wa chama chake waruhusiwe kuingia mahakamani.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai imemtaka aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kufika ofisini hapo kutoa maelezo au ushahidi kuhusiana na tuhuma anazozitoa kwa umma kupitia mitandao ya kijamii.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imemuondoa mgombea urais kupitia Chama cha ACT – Wazalendo, Luhaga Mpina kwenye mbio za urais, baada ya pingamizi lililowekwa dhidi yake na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari kukubalika.
Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Upinzani, CHADEMA, Tundu Lissu yanayohusiana na usikilizwaji wa kesi ya uhaini inayomkabili.
Mgombea mwenza wa Chama tawala nchini Tanzania, CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi amemtaka mwanasiasa aliyeenguliwa kwenye nafasi ya kugombea urais kupitia chama cha
Hali ya kibinadamu katika mji wa El-Fasher nchini Sudan inazidi kuzorota baada ya mashambulizi mapya ya vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) yaliyosababisha vifo, utekaji na uharibifu mkubwa. Madaktari wamesema watu wasiopungua 13, wengi wao wanawake na watoto, waliuawa waliposhambuliwa wakiwa barabarani karibu na mji wa huo mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.
Chama cha Mapinduzi (CCM), moja ya chama kikongwe barani Afrika kinajiandaa na uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, miongoni mwa maandalizi hayo ni kupata wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, huku wakiwa na uhakika kuwa Rais wa sasa wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ndiye mgombea wao katika nafasi ya urais.
Waandamanaji wamekusanyika katika makutano na maandamano kote Israel asubuhi ya leo, wakishinikiza kusitishwa kwa kampeni ya kijeshi ya Israel huko Gaza na kurejeshwa kwa mateka waliosalia wanaoshikiliwa na Hamas.
Ni mwaka mmoja sasa tangu wanaharakati na wanachama wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania, CHADEMA Deusdedith Soka, Jacob Mlay and Frank Mbise, watoweke katika mazingira ya kutatanisha mnamo Agosti mwaka 2024.